|
Karume Ataka Tatizo La Kujaa Maji Lipatiwe Ufumbuzi
|
||||||||||
|
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume ameushauri uongozi wa Baraza la Manispaa Zanzibar, kuchukua hatua kutatua tatizo la kujaa kwa maji katika maeneo mbali mbali ya mji wa Zanzibar, taarifa ya Ikulu imeeleza. Rais Karume alitoa ushauri huo jana, wakati akitembelea maeneo yaliyoathiriwa na mvua kubwa katika mji wa Zanzibar. Rais Karume katika ziara hiyo alifuatana
na Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa, Mabrouk Jabu na Mkuu wa Mkoa Mjini
Magharibi, Abdalla Mwinyi, pamoja na wataalamu Alisema kuwa amesikitishwa sana na mtatizo
yaliyowakumba wananchi waliofikwa na maafa hayo, kutokana na mvua kubwa
zilizonyesha kwa wastani wa masaa 35, kuanzia juzi hadi jana asubuhi.
Katika ziara hiyo, Rais Karume pamoja na tatizo la kunyesha mvua kubwa ambavyo haijapata kunyesha kwa karibu ya miaka kumi iliyopita, alielezwa kuwa moja katika matatizo makubwa yalisababishwa na tatizo la kuja maji ni hitilafu za michirizi na ujenzi holela. Ilifahamika kuwa, aidha michirizi ilidhihirika kuwa na uwezo mdogo wa kuondosha maji au vikwazo vya makusudi vilivyotokana na baadhi ya wananchi kuweka vizuwizi vya maji, kutokana na ujenzi holela katika baadhi ya maeneo ambayo maji hutuama kwa wingi. Rais Karume alitembelea maeneo ya Mwanakwerekwe, Darajabovu, Sebleni, Jang'ombe, Mazizini na Kariakoo ambapo mamia ya wananchi waliathirika kutokana na mvua hizo, hadi kufikia wengi miongoni mwao kuhama makaazi yao au nyumba zao katokana na athari za kujaa maji. "Tumelazimika kuhama kwa sababu maji mengi yamejaa ndani tunaomba tusaidiwe haya maji tu kuondolewa, kwani tunasumbuka", walieleza wananchi wakati Rais Karume akikagua baadhi ya wananchi waliokubwa na maafa hayo huko Sebleni. Katika baadhi ya maeneo maji yalijaa kwa kiasi kikubwa hata kusababisha tatizo la usafiri, tatizo hilo limejitokeza zaidi katika barabara ya eneo la Mwanakwerekwe kuelekeo Fuoni. Hata hivyo, katika maeneo mengine ya mji, maji mengi yaliyotuwama katika mitaa na kusababisha athari za hitilafu ya umeme. Hata hivyo, juhudi zinachuliwa ili kuhakikisha watu walioathirika wanapatiwa misaada inayohitajika kama makaazi ya muda na dawa.
PRESSS RELEASE Abdulla A. Abdulla
Zanzibar, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF limeitikia wito wa Kamati ya Taifa ya Maafa kusaidia wananchi waliopatwa na maafa ya mafuriko ya mvua za masika zilizoathiri sehemu nyingi hapa Zanzibar. Akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, leo hapo afisini kwake Vuga. Mkuu wa Shirika hilo katika Afisi ndogo ya hapa Zanzibar Bw. FRANCOIS RUMECI alisema ameitika wito wa Serikali kuangalia namna watavyoshirikiana na Serikali katika kusaidia kukabiliana na maafa hayo. Alisema amevutiwa sana na hatua za haraka za Serikali kwa mwamko wake wa kulishughulikia suala hili na kulipa uzito unaostahili. Aliwapongeza viongozi wa Kitaifa Mhe. Rais wa Zanzibar na Waziri Kiongozi kwa kujali maisha ya wananchi wao kwa hatua zao za haraka za kufuatilia masuala hayo.. Mwakilishi huyo wa UNICEF hapa Zanzibar alisema atatuma mtaalamu wao kufuatilia katika maeneo husika na tayari ameshaiarifu Afisi Kuu Dar es Salaam ambako anatarajia kupata msaada mdogo wa kuanzia. Akitoa shukrani zake kwa Shirika hilo Mhe. Waziri Kiongozi alisema anawashukuru kwa kuitika wito huo kwa haraka na nia yao ya kusaidiana na Serikali katika kushughulikia maafa hayo. Mheshimiwa Nahodha alisema ingawa bado tathmini kamili ya maafa hayo haijapatikana kutokana na baadhi ya watu kutoripoti katika vituo vilivyowekwa, lakini timu ya wataalamu inafuatilia katika maeneo husika ili kupata taarifa kamili. Alisema wataalamu hao inawawia vigumu kumfuata mtu mmoja mmoja, lakini watu waliofika vituoni wameshaanza kuhudumiwa na alisema kuwa madawa ya tiba na ya kusafisha maji ya kunywa ni miongoni mwa mahitaji yanayotakiwa kwa haraka sana. Aidha, zaidi ya misaada ya madawa alitaja hasara za miundo mbinu iliyoharibika kama daraja la Mwanakwerekwe ambalo limekatisha mawasiliano ya barabara baina ya mjini na vitongoji fuoni hadi Wilaya ya Kusini kuwa ni miongoni mwa gharama kubwa ambazo Serikali haiwezi kuzimudu kwa haraka. Wakati huo huo kuna habari zisizothibitishwa
kuwa baadhi ya sehemu katika maeneo ya Nyerere watu wawili wamegundulika
kuwa na maradhi ya tumbo la kuharisha ambayo inaminika kuwa walikunywa
maji yasio salama.
|
Press Release
on Chief Minister |
|||||||||
|
|
||||||||||
| President Karume speaks to the people on Eid. |
![]() |
|||||||||
|
|
||||||||||
| 41st Revolutionary Day is celebrated |
![]() |
|||||||||
|
|
||||||||||
| Maelfu washiriki upandishwaji Bendera |
![]() |
|||||||||
|
|
||||||||||
|
Government Statement on CUF Complaint to UN Disclosure of Environmental and Social Assessment Framework Tagazo Kuanzishwa Mfuko Maalum Wa Kuendeleza Viwanda Vidogo Vidogo Na Vya Kati ZANZIBAR GOVERNMENT
|
||||||||||
|
Closure statement of the 19th Session of the house of Representatives BARAZA
LA WAKILISHI
|
||||||||||
|
|
||||||||||
![]() |
||||||||||
|
MORE ARTICLES
Karume
Shuffles cabinet: Zanzibar Permanent Voter registry book starts November Karume wants People to cooperate with Police Karume tells Seif Sharif Hamad not to LIE to the People The Houseof Rep. gives a CUF legislator 1 Yr. Suspension The
Zanzibar Kyenote Address by H.E Shamsi Vuai Nahodha
|
||||||||||
| Archieves | ||||||||||
|
|
||||||||||
|
|
||||||||||
|
|
||||||||||
|
|
|
|||||||||